Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na
uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza.
Bio Bus,lenye viti 40 na ambalo linatoa huduma ya uchukuzi
kati ya Bath na uwanja wa ndege wa Bristol ,linaweza kusafiri hadi maili 186
kwa kutumia tangi moja la gesi.
Gesi hiyo hupatikana kupitia kutibu maji taka na uchafu wa
chakula usiofaa kwa matumizi ya binaadamu.
Uchafu unaopatikana katika abiria wa basi moja unaweza
kutumiwa kutoa kawi ya kulisafarisha basi hilo kutoka Lands End hadi John
O'Groats.
Basi hilo ambalo limepewa majina kadhaa ya kutungwa likiwemo
lile la Basi la pili linapongezwa kama njia mojawapo ya kuchochea usafiri wa
uma huku ukiimarisha ubora wa hewa jijini.
Gasi inayotumiwa kuliendesha gari hilo hutoka katika mradi
wa maji taka wa Bristol ambao husimamiwa na GENeco ambyo ni kampuni tanzu ya
Wassex Water.
Mohammed saddiq,meneja mkurugenzi wa kampuni ya GENeco
,anaamini chakula na maji taka yanaweza kutoa kawi ya Biomethane inayotoa gesi
katika shirika la kitaiafa la gesi inayoweza kutoa gesi yenye uwezo wa kutumika
katika nyumba 8,500 mbali na kuliendesha basi hilo la Bio.
No comments:
Post a Comment