Kocha wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema Angel
Di Maria alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa wanaighalimu sana timu
hiyo haswa inapokuwa uwanjani kutokana na tabia yake ya kupoteza mipira mara
kwa mara na ndio maana haikuwa tabu sana kwake hata mabosi wa klabu yake kuamua
kumruhusu aondoke klabuni hapo.
Lakini pia kocha huyo aliongeza kuwa ujio wa James
Rodriguez, aliyesajiliwa kwa ada ya Euro milioni 80 kutokea pale klabu ya Monaco mara baada ya kumalizika kwa michuano
ya kombe la Dunia kumefanya kutokuwa na mahitaji tena ya kuwa na Di Maria kwani
anaonekana kufiti sana katika nafasi aliyokuwa akiitumikia Muajentina huyo.
Ancelotti amesema tabia ya Di Maria kupoteza mpira na aina
yake ya uchezaji haswa linapokuja suala la michezo migumu ilikuwa ikiighalimu
sana timu hiyo kwani wakati mwingine alikua akipoteza pasi nyakati muhimu.
No comments:
Post a Comment