Pages

Tuesday, November 18, 2014

HUZUNIII:: AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA

 Stori:  Hamida Hassan na Gladness Mallya
Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar,  juzi kati alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.
Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa akidai kunyanyaswa.
 AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA
Baada ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta ya taa alipoona maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.


Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
 “Ndugu zangu naomba mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi nilichokuwa nimekunywa.

“Yote haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa babu yangu ambaye alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati nilikuwa na matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.

Aliongeza: “Niliwahi kukutwa na ajali mbaya ambayo ilisababisha niende kuishi nyumbani kwa bibi yangu ambapo babu amekuwa kero. “Awali nilipofika nyumbani sikumkuta babu lakini alipofika akawa kero kwangu kwani ni mtu anayetaka nimpe hela kila kukicha, nilikuwa nikienda kuhangaika napata elfu ishirini nampa elfu kumi na tano na mimi naweka elfu tano kwa ajili ya kujipanga ili nikapange chumba.
ALIAMBIWA AKICHELEWA ATAFUNGIWA MLANGO
“Siku ya tukio nilimuaga naenda kwa baba yangu mdogo kumsalimia akaniambia nikirudi usiku nitakuta amefunga mlango nitafute pa kwenda kulala.

“Kweli, niliporudi alianza kuninyanyasa kwa maneno, ugomvi wetu ukawa mkubwa nikaona bora nijiondoe duniani kwani siwezi kuendelea kuishi maisha ya manyanyaso kama haya,” alisema Nicholas kwa shida kutokana na majeraha aliyonayo mwilini hasa usoni na mikononi.Nicholas Mhagama akiuguza majeraha hospitalini.

Akizungumza kwa njia ya simu bibi wa kijana huyo, Bi. Mhagama alikiri kwamba ni kweli huyo babu ambaye yeye anamuita shemeji amekuwa akimnyanyasa sana Nicholas. “Ni kweli amekuwa akimfukuza nyumbani hapo wakati siyo kwake na siku ya tukio baada ya kuona ugomvi umekuwa mkubwa nilikimbilia kwa mwanangu huko Kimara.

“Ugomvi kati ya babu yake huyo mdogo  na huyu Nicholas ulianza saa tatu usiku. Nilipoona kero niliamua kutimkia Kimara kwa mwanangu,” alisema bibi huyo.

SIMU YA MOTO YAPIGWA USIKU
“Ilipotimia saa nne usiku nikapigiwa simu na kufahamishwa kuwa Nicholas kajilipua kwa mafuta ya taa.

BABU ORIJINO ALISHAFARIKI
“Mume wangu (Babu orijino) alishafariki na huyu Nicholas kweli kabisa huwa anagombana na  huyo babu ambaye ni shemeji yangu. “Kisa cha ugomvi wao ni kumpa manyanyaso ya hali ya juu, nawaomba mumsaidie huyo kijana, naombeni jamani,” alisema bibi huyo.


Juhudi za kumpata babu huyo anayedaiwa kumnyanyasa mjukuu wake hazikuzaa matunda.CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment