Spika wa Bunge , Anne Makinda.
Nimshukuru Mungu kwa kuniweka hai mimi na wewe msomji wa makala haya, hakika hatuna budi kumshukuru milele.
Wiki iliyopita gumzo la mjini au pengine nchini lilikuwa sakata la
akaunti ya Tegeta Escrow ambapo kuna madai kuwa kuna mabilioni ya fedha
‘wakubwa’ wamezichota bila hata kulipia kodi ya nchi.
Zimetajwa kuwa ni shilingi bilioni 306! Ni fedha nyingi sana ambazo eti kuna watu wamegawana! Siamini mpaka niaminishwe kwa ‘data’ zisizo na mashaka yoyote.
Zimetajwa kuwa ni shilingi bilioni 306! Ni fedha nyingi sana ambazo eti kuna watu wamegawana! Siamini mpaka niaminishwe kwa ‘data’ zisizo na mashaka yoyote.
Ajabu ni kwamba kuna wakati nilisikia baadhi ya viongozi na watendaji
wa serikali akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wakidai kwamba
kiasi cha dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo
katika ‘Tegeta Escrow Account’ si za serikali, hivyo si mali ya umma.
Lakini nilichanganyikiwa zaidi baada ya kusikia ikisemwa kuwa akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Kampuni ya Independent Power Limited (IPTL)! Nilipigwa na bumbuwazi, vipi fedha ambazo siyo za umma zinafunguliwa akaunti na vyombo vya serikali?
Lakini nilichanganyikiwa zaidi baada ya kusikia ikisemwa kuwa akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Kampuni ya Independent Power Limited (IPTL)! Nilipigwa na bumbuwazi, vipi fedha ambazo siyo za umma zinafunguliwa akaunti na vyombo vya serikali?
Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea
kurudia kuueneza huo usemi kwamba fedha hizo si mali ya umma.
Inasikitisha pia kwamba baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa navyo
vikibeba na kusambaza maelezo hayo bila kuhoji na kuchunguza.
Inashangaza sana kuona asasi za kiraia nazo zimekaa kimya juu ya jambo
hilo zito.
Nilisikia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza
kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta Escrow
iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo
fedha za umma.
Mimi naamini kwamba kamati hiyo ya PAC ilifanya hivyo kwa kuwa kuna
fedha za umma ndani yake vinginevyo ingekuwa haina sababu yoyote ya
kufuatilia fedha za watu binafsi. Niwakumbushe tu wasomaji wa safu hi
kwamba mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC)
ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la
POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za
Tanesco.
Akaunti ya ‘Tegeta Escrow’ ilifunguliwa kutokana na kuwapo
kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa
na IPTL na kuuzwa kwa Tanesco. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa
(ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha
kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa
kwa IPTL.
Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye
akaunti hiyo maalumu ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco
baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.
Kwa mujibu wa PAC , hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Desemba 2012
za Tanesco zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la
umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100?
Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100?
Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika
lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unafanana kwa kila hali na huu wa
sasa wa ‘Tegeta Escrow’.
Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge David Kafulila alisema kwamba Jaji
Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha
kutoka akaunti ya ‘Tegeta Escrow’. Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa PAC
anasema amepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba
hakuna popote alipotaja akaunti ya ‘Escrow’.
Hata hivyo, alipopitia muhtasari wa kikao kati ya Tanesco, IPTL na
Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza alikuta
wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za ‘Tegeta
Escrow’ zipewe Kampuni ya PAP.
Zitto anakwenda mbali zaidi na kudai kwamba wote waliohudhuria kikao
hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu Tanzania,
wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria
zilizopo.
Lakini nami najiuliza kama hivyo ni kweli, inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha wizara?
Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), katika
ripoti yake iliyofika bungeni imefichua ukweli wa sakata hili . Bunge
chini ya Spika, Anne Makinda (pichani), lina kila sababu kupitia sheria
yake kujadili hoja hii ili ukweli ubainike kama ulivyoapa na tuondoe
hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya
kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa, jibu lipatikane,
shilingi bilioni 306 zimeliwa? Au kodi ya nchi nayo imeliwa?
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
No comments:
Post a Comment