Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ni miongoni mwa
viongozi wa Tanzania ambao wakisimama sehemu yoyote kuzungumza lazima mwandishi
yeyote ataiweka kalamu yake vizuri kujua lazima mazito ya kuwafikishia Wananchi
yawepo.
Kwenye bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania November 11
2014 Dr. Mwakyembe amezungumzia ishu 7 kuhusu usafirishaji kwa njia ya reli
Tanzania.
1 ‘Tumewezeshwa na serikali kuunda upya vichwa vinane vya
Treni kwenye karakana yetu ya Morogoro, ndio unaona sasa hivi Treni zikipita
vinafanya kazi, tumeingiza vichwa vingine nane karakana ya Morogoro vitatoka
mwezi wa tano’
2 Benki ya dunia sasa hivi tunaanza mchakato tunapata vichwa
vitatu vipya pamoja na Mabehewa 44 kuanzia Dar es salaam kwenda Isaka, Mamlaka
ya bandari baada ya kuona benki ya dunia inaleta vichwa vitatu nayo imetafuta
vichwa vitano vya treni navyo vinaingia karakana ya Morogoro.
3 Tumenunua Mabehewa mapya ya mizigo 274 tunaanza kuyapepea
mwezi huu bandari ya Dar es salaam, ni bunge hilihili ambalo limeniruhusu ndani
ya mwaka huu wa fedha tuagize Mabehewa mengine ya mizigo 204.
4 Tumenunua vichwa vingine vya Treni 13 navipokea January
2015 na vilevile bunge hili limeruhusu tununue vichwa vingine 11 ndani ya mwaka
huu wa fedha.
5 Tumenunua Mabehewa 22 mapya ya abiria, nataka tu kutoa
agizo kwa Mamlaka ya reli kwamba tutakapopata Mabehewa 22 ya abiria January
2015, ratiba ibadilike sasa tuwe na safari tatu kwa wiki za Treni ya abiria
kuanzia Dar es salaam kwenda bara na kutoka bara kuja Dar es salaam na mwezi wa
nne tutakua na Treni ya abiria mara nne kwa wiki.
6 Reli yetu ni ya zamani sana ina umri wa zaidi ya miaka 100
mnajua, inahitaji matengenezo makubwa na wengi wanasema si mngeing’oa tu hiyo
muweke reli mpya? sawa lakini kuing’oa reli iliyopo na kujenga nyingine mpya
hautakuwa uamuzi mzuri sana manake tutakwamisha uchumi wa nchi yetu.
7 Ni kweli tunajenga reli nyingine ya pili na tuko kwenye
harakati za kutafuta pesa na itajengwa kwenye kordo hiyohiyo ya reli kuanzia
Dar es salaam kwenda Kigoma, Mwanza, Mpanda na sasa tunaongeza mpaka Kalema….
huu ni mradi mkubwa sana na utagharimu nchi zaidi ya dola za kimarekani Bilioni
7.6
No comments:
Post a Comment