Pichani kiijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya
Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12. Assalam
Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada unahitajika
kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar,
amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na
ajali kugongwa na Vespa kwa muda wa siku
nyingi tu, walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana
kupata
matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu
kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.
Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na
maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala
inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam
picha inavyojionyesha.
Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa
msaada wenu kwa ajili ya kuweza kumpeleka nchini India kwaajili ya matibabu na
kumgharamikia mtu wa kufuatana nae katika familia, kutokana na gharama ni kubwa
na uwezo ni mdogo.
Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande
wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu
Suleiman Othuman kwa hali na mali.
Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka
kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
Namba zake za simu ni-:
255777489015
Tigo: 255655489015
Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog ya Abou Shatry Number 301-278, 3977, Email
swahilivilla@gmail.com
No comments:
Post a Comment