Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 20, 2014

KINANA ASHIRIKI KILIMO KATIKA SHAMBA LA WANANCHI KIJIJI CHA MKOTOKUYANA NACHINGWEA

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe wakati alipowasili katika kijiji cha Nkotokuyana jimbo la Nachingwea katika mwendelezo wa ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara itakayomchukua siku 16 akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na srikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi katika vijiji mbalimbali , Majimbo na wilaya Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NACHINGWEA-LINDI) 3 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu kuwasili katika kijiji cha Mkotokuyana 


4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliiza Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya kufika kwenye shamba la ufuta alilolikagua leo kijijini hapo, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi 5
Baadhi ya akina mama wanakikundi hichi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM huku wakiwa wameshika majembe yao. 6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa jimbo la Nachingwea wakikagua shamba la Mkotokuyana 7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kilimo katika shamba hilo huku Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe akiwa amepanda akishuhudia kazi hiyo. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi 9
Pamoja na vumbi kubwa kutimka wakati akifanya kazi hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliendelea na kazi. 10
Kilimo kimepamba moto 16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Naipanga Nachingwea. 15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Naipanga 14
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jiko la shule ya Sekondari Nachingwea High School. 12
Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathiasa Chikawe akishiriki katika kusafisha shamba la ufuta katika kijiji cha Mkotokuyana. 11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la wananchi la kijiji cha Mkotokuyana wilayani Nachingwea leo.

No comments:

Post a Comment