Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia)
akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine
ni Kizza, Javu na Coutinho
kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo
Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa
akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika
jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa
katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji
huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari
na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba
iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi
kumsajili basi moja kwa moja ataingia
makubaliano na klabu ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano
ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.
No comments:
Post a Comment