Pages

Tuesday, November 18, 2014

KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM CHAWASILI KATIKA BANDARI YA DAR KITAZAME HAPA



Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
Taaswira ya Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya Meli kabla ya kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Eng. Japhet Masele kuhusu vitu mbalimbali ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Marcellin Magesa kwa kazi nzuri ya upatikanaji wa Kivuko hicho kipya na cha kisasa cha MV Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa ndani ya chumba cha Nahodha wa Kivuko hicho.
Mhandisi Masele akitoa maelezo kuhusu kamera maalumu kwenye Kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua boya la kujiokolea ndani ya siti mojawapo ndani ya Kivuko hicho kipya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Marcellin Magesa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe wakiteta jambo kabla ya kuwasili kwa kivuko hicho kipya .
Waziri wa Ujenzi akishuka kwenye ngazi mara baada ya ukaguzi huo.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) Wizara ya Ujenzi.

No comments:

Post a Comment