Pombe inatakiwa kuwa na nembo inayoonyesha kiwango cha kalori
au kipimo cha joto litolewalo na chakula ili kupunguza vitambi au unene wa
kupita kiasi.
Madaktari wa afya ya umma, wameonya kuwa glasi kubwa ya
mvinyo inaweza kuwa na kiasi cha kalori 200- sawa na donati, aina ya maandazi.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu hawajui madhara ya kula
kiwango kikubwa cha kalori.
Waziri wa Afya Jane Ellison amesema "hatua kubwa"
imefanyika kwa kuviwekea nembo vyakula, na kwa suala hilo serikali
italiangalia.
Sekta ya vinywaji imesema imesema iko tayari kwa wazo hilo
la kuweka nembo zenye kuonyesha kiasi cha kalori, lakini kuweka nembo
zinazonyesha kiwango cha kilevi katika kinywaji ni muhimu zaidi.
Uingereza ni moja ya mataifa yenye watu wenye unene wa
kupita kiasi duniani kwa kuwa na idadi ya karibu robo ya watu wazima kuwekwa
katika kundi la wenye unene wa kupitiliza.
Vyakula tayari vinakuwa na taarifa za kiasi cha kalori
kilichomo ndani yake, lakini pombe haimo katika sheria za Umoja wa Ulaya
zinazotaka vyakula viwekewe nembo.
Mvinyo nao watakiwa kuonyesha kiwango cha kalori
Na Tume ya Ulaya inaangaliwa iwapo vinywaji viwekewe nembo
yenye kuonyesha kiasi cha kalori kilichomo.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Masuala ya Afya ya Jamii
nchini Uingereza, umesema hatua hii itaungwa mkono na wanywaji nchini
Uingereza.
Mkuu wa chama hicho cha RSPH, Shirley Cramer, ameiambia BBC:
"Ni jambo la kushtusha kweli - asilimia 80% ya watu wazima hawana wazo la
kujua kiasi cha kalori kilichomo katika kinywaji chochote na kama wanafikiri
wana wazo hilo kwa ujumla wanakadiria kiasi cha chini mno."
"Itasaidia taifa kupunguza watu wenye unene wa
kupitiliza na huenda kupunguza kupunguza unywaji wa pombe."
Kiasi cha kalori:
Glasi kubwa ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 8%
ni kalori 170 Kiasi hicho hicho cha glasi ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha
asilimia 14% ni kalori 230 Painti moja yenye asilimia 4% ya bia ni zaidi ya
kalori 180
No comments:
Post a Comment