Pages

Friday, November 21, 2014

Korea Kaskazini kufanya jaribio la nuklia

Korea Kaskazini imetishia kufanya majaribio ya zana zake za nuklia katika jibu lake kwa vitisho vya umoja wa Mataifa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.
Taarifa kutoka kwa wizara yake ya mambo ya nje ilishutumu Marekani kwa kuchochea umoja wa Matifa kuchunguza visa vya ukiukaji wa haki za binadfamu nchini humo hivi majuzi.
Korea Kaskazini iliwahi kufanya majaribio ya zana zake za nuklia mwaka 2006,2009 na 2013.\


Vitisho vya nchi hiyo vinakuja huku picha za satelite zikionyesha kuwepo shughuli nyingi tu katika kiwanda cha nuklia nchini humo.
Kamati ya umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, ilipitisha azimio lililokuwa linatoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kusihitaki Korea Kaskazini kwa mahakama ta kimatifa ya ICC kwa tuhuma za kukiuka haki za binadamu.
Pyongyang ilisema kuwa azimio hilo, lilitokana na ushahidi wa uongo na porojo dhidi ya serikali.
''Azimio hilo lililoshinikizwa na Marekani,lilikuwa hatua ya kuingilia uhuru wa taifa hili na inatuwacha bila budi la kufanya jaribio la nuklia kwa mara nyingine,'' ilisema taarifa ya serikali.

Taarifa hio iliongeza kusema jeshi litakuwa tayari kwa chochote dhidi yake na sanasana ikiwa kutakuwa na shambulizi dhidi ya nchi hiyo kutoka kwa Marekani.

No comments:

Post a Comment