Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 11, 2014

MAZISHI YA KITAIFA ZAMBIA


Zambia inafanya mazishi ya kitaifa ya Rais Michael Sata ambaye alifariki dunia mwezi uliopita katika hospitali moja nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 77. Maelfu ya watu wamehudhuria misa maalum iliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka. Viongozi mbalimbali wa kimataifa ni miongoni mwa waliohudhuria. Akijulikana kama "King Cobra" kutokana na matamshi makali, Rais Sata alichaguliwa kuwa rais mwaka 2011. Nchi hiyo kwa sasa inaendeshwa na kaimu rais, na uchaguzi utafanyika mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment