Pages

Sunday, November 9, 2014

MBEYA CITY YAENDELEA KULA KISAGO YACHAPWA 1-0 NA STAND UNITED


Kwa mara ya kwanza ikicheza nyumbani Stand United hii leo imeonja utamu wa ligi kuu soka Tanzania bara mara baada ya kupata ushindi wake wa kwanza ndani ya ligi hiyo kwa kuifunga Mbeya City 1-0 mchezo ukichezwa dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Mashabiki wa Mbeya City walikuwa na mbwembwe kiasi cha kuliweka kiganjani dimba hilo nao mashabiki wa Stand wakiwa kama wamenyeshewa mvua kwa muda wa takribani dakika 45 za kipindi cha kwanza na dakika kama 15 za kipindi cha pili lakini mambo yalibadilika baada ya hapo furaha yao ikageuka kuwa kilio.

 
Mbwembwe mwanzo mwisho...lakini mwisho wa mchezo Mbeya City wanatoka vichwa chini...
Dakika ya 76 Shangwe za mashabiki wa Stand United zatawala safari hii zikiwa na maana zaidi baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Chibibiere Abisalum, ambaye ni raia wa Nigeria kupasia mpira kambani akipokea pande safi toka kwa Musa Said Kimbu aliye wapunguza mabeki wa Mbeya City. Picha kwa hisani ya G Sengo Blog

No comments:

Post a Comment