Pages

Wednesday, November 19, 2014

MDAU ANDREW CHALE KUTOA VITABU VYA MAISHA YAKE‏

Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Mjengwa  wa Mjengwa blog
Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog.
..Ni vya 'Who Is Andrew Chale', 'Nimnukuu Nani?' na ''Mimi ni Historia',
Na Mwandishi Wetu
Mwandishi wa Habari nchini Tanzania, Andrew Chale anayeandikia magazeti ya Tanzania Daima na Sayari yanayotolewa na kampuni ya Free Media ya jijini Dar es Salaam, ambaye pia mwandishi 'msaada' wa blog za habari mbalimbali za hapa nchini na nje ya Tanzania ameanza mchakato rasmi wa kuandika vitabu vitatu (3) vitakavyokuwa vikielezea juu ya Maisha yake.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Novemba 19, Andrew Chale alibainisha juu ya kusudio hilo la kutoa Vitabu vya kuelezea Maisha yake ni ndoto aliyonayo kwa miaka mingi na kwa sasa imetimia.


"Wengi watajiuliza sasa nimepata wapi ujasiri wa kufanya jambo hili kubwa la kuelezea Maisha yangu?.Ni rahisi sana, Unapokuwa na Mungu kila jambo linawezekana hivyo vitabu hivi vitakuwa ni muongozo kwa Vijana wote hapa Duniani kuelewa kuwa yale yote wanayopitia si ya kuyakatia tamaa, bali kuangalia wapi wataweza kujikomboa na hata kuendana na hali iliyopo kwa kujithamini, kujielewa, uvumilivu na kufikia malengo stahiki ya maisha" alifafanua Andrew Chale.
Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni: "Who Is Andrew Chale?" Sehemu ya Kwanza), 'Who Is Andrew Chale 2?"- 'Nimnukuu Nani?' (Sehemu ya Pili) na Kitabu cha mwisho kitakachojulikana kama "Mimi ni Historia".
Akifafanua vitabu hivyo vya 'Who Is Andrew Chale' cha kwanza na kile cha pili cha 'Who Is Andrew Chale 2- 'Nimnukuu Nani?', alibainisha kuwa vitaelezea kwa kina Historia yake tokea kuzaliwa hadi alipofikia sasa huku cha Pili cha 'Who Is Andrew Chale 2-'Nimnukuu Nani' kikielezea yale mambo yote yaliyojificha nyuma ya pazia na ukakasi wa maisha aliyopambana nayo kutoka kwa walimwengu na mwishowe anauliza "Nimnukuu Nani?".
10379994_679143752122499_6894615982670728862_o
Aidha,kwa upande wa kitabu cha : "Mimi ni Historia" ameweza kuelezea ujumbe juu ya Vijana kutokata tamaa na baadala yake wasonge mbele kwa magumu yote waliyopitia, ikiwemo yeye.
"Mimi ni Historia", mimi mwenyewe naogopa sana, kwanza kuanzia jina la Kitabu, Nakumbuka nilimuuliza Mama yangu Mzazi juu ya jambo fulani la kifamilia baina yake na Baba, lakini jibu alilonipa ndilo lililonifanya nishike neno hili 'Mimi ni Historia'. Kikubwa kwenye kitabu hichi nitafafanua mambo mbalimbali ya kihistoria bila shaka hata atakayesoma ambaye alipitia mambo kama yangu naye itakuwa ni Historia" alimalizia Andrew Chale.
Vitabu hivyo vyote vitajaa Historia ya kweli, itakayotoa mafunzo kwa kila mmoja atakayebahatika kuvisoma Pia vitakuwa ni kama mafunzo, mfano wa kuigwa, na kukuacha ki mdomo wazi na hata kububujikwa machozi.
Aidha, Andrew Chale, aliomba ushirikiano kwa wadau kujitokeza kumsapoti ilikufanikisha juhudi za vitabu hivyo ikiwemo gharama za kuandaa Mswada, mapitio na uchapaji.
"Kwa sasa nipo katika andalio la Simulizi, na lengo kuu nije nichapishe Mkuki na Nyota.Kwa sasa natafuta watu watakao kuwa msaada wa awali wa kufanikisha dhumuni langu hili Ikiwemo ushahuri, msaada wa kifedha, mchango wa kimawazo na mengineo. Tuwasiliane kupitia 0719076376 au 0767076376 au 0688076376 au chalefamily@yahoo.com" alimalizia Andrew Chale.
Andrew Chale, ambaye kwa sasa anaishi Bagamoyo, Mkoani Pwani akifanya shughuli zake hizo za Uandishi wa Habari, Pia ni Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini, msanii wa masuala ya Vichekesho, Mtunzi wa filamu, maigizo na mshahuri kwenye matamasha ya sanaa na Muziki, mbali hayo pia ni Mjasiriamali katika Sanaa na Utamaduni ikiwemo kukuza Sanaa na Utamaduni kwa Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment