Mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Barcelona Lionel AndrĂ©s "Leo" Messi Cuccittini amekuwa wa kwanza kuifikia rekodi ya ufungaji mabao mengi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, iliyokuwa inashikiliwa na aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid pamoja na Schalke 04 ya nchini Ujerumani RaĂºl GonzĂ¡lez Blanco.
Messi ameifikia rekodi hiyo usiku wa kuamkia hii leo baada ya kuifungia Barcelona mabao mawili katika mchezo wa mzunguuko wa nne wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdam uliochezwa huko Amsterdam Arena.
Kabla ya mchezo huo Messi alikua ameshafunga idadi ya mabao 69 katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya upande wa vilabu na alikua akihitaji mabao mawili ili kuifikia rekodi ya mabao 71 ambayo iliwekwa na Raul akiwa na klabu ya Schalke msimu wa 2010–11.
Hata hivyo Messi amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kucheza michezo 90 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ikiwa ni tofauti kubwa na Raul ambaye alifikisha mabao 71 baada ya kucheza michezo 144, huku Cristiano Ronaldo mwenye mabao 70 ameshacheza michezo 107.
Messi pia ameweka rekodi ya kufikia rekodi hiyo akiwa na umri mdogo wa miaka 27 tofauti na wapinzani wake ambapo Rul aliweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 34 na aneyemfuatia kwa sasa Ronaldo ana umri wa miaka 29.
No comments:
Post a Comment