Pages

Sunday, November 23, 2014

MESSI APIGA HAT TRICK BARCELONA IKIICHAPA SEVILLA 5-1, AFIKISHA MABAO 252

Wachezaji wa Barcelona walilazimika kumbeba nahodha wao,Lionel Messi baada ya kufunga bao la tatu, hat trick na kuisaidia Barca kuitwanga Sevilla kwa mabao 5-1.

Katika mechi hiyo ya La Liga iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Messi alionyesha kuvunja rekodi iliyowekwa na Telmo Zarra.
Nyota huyo wa zamani wa Athletic Bilbao aliyetamba kati ya mwaka 1940 na 1955 alimaliza La Liga akiwa amefunga mabao 251.
Kwa mabao matatu ya Messi dhidi ya Sevilla, amefanikiwa kufikisha 252 na pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi La Liga akiwa na miaka 27 tu.




No comments:

Post a Comment