Mhubiri wa kimataifa na motivational speaker wa Marekani Dr Myles Munroe aliyekuwa nchini Tanzania hivi karibuni, amefariki dunia kwa ajali ya ndege pamoja na watu tisa wengine akiwemo mke wake na binti yake.
Ajali hiyo ya ndege yake binafsi imetokea huko Bahamas.
Kwa mujibu wa gazeti la The Bahamas Tribune, ndege yake ilianguka wakati ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Grand Bahamas huko Freeport. Alikuwa akienda kuhudhuria kongangamano la Global Leadership lililokuwa lifanyika kuanzia November 10 hadi 13.
Dr Munroe aliyekuwa na miaka 60 ameshaandika machapisho zaidi ya 100 ya dini na ushauri na ametembea katika nchi zaidi ya 130. Vitabu vyake 49 viliuza zaidi.
Katika ziara ya Afrika alitembelea nchi 9 zikiwemo Tanzania na Kenya.
No comments:
Post a Comment