Pages

Friday, November 7, 2014

MWAKILISHI MKAZI WA UNDP NCHINI ATAKA WANANCHI WA VIJIJINI WASAIDIWE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI‏

IMG_4025
Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipotembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara yake ya siku mbili mara baada ya kuwasili wilayani humo. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu aliyeambatana na Mwakilishi huyo.


Na Mwandishi wetu,
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wadau wa mazingira nchini kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji kutumia nguvu na rasilimali walizonazo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuendelea kuhifadhi mazingira na viumbe vilivyopo wakiwemo wanyamapori
Bw, Rodriguez aliyasema hayo wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo .
Akizungumza baada ya kutembelea na kuzindua mradi wa kuwawezesha wafugaji wa wilaya ya Longido kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kujenga uzio wa kulinda mifugo yao na wanyama wakali Bw, Rodriguez, amesema kutokana na uelewa mdogo wa mabadiliko yanayoendelea kutokea wananchi wengi wa vijijini wanahitaji msaada wa namna ya kuyadhibiti.
IMG_4027
Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akiendelea kutoa maelezo kwa Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez (katikati), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya.
Aidha alisema kwa sasa wananchi wengi wanatumia muda na nguvu nyingi kushughulikia matokeo ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na maeneo mengi wamekuwa wakijikuta wanagombana wenyewe kwa wenyewe badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya msingi.
"mara nyingi wananchi wa vijijini kama hawa wafugaji mmekuwa wamekuwa wakilaumiwa kwa matokeo ya yale wanayoyafanya kwa kusukumwa na mabadiliko haya na mengine wangeweza kuyajua wala wasingeyafanya "alisema Rodriguez.
Aidha Bw. Rodriguez ambaye pia ni Mkuu wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na shirika hilo hapa nchini amewataka viongozi na watendaji wakiwemo watalaam kutumia muda na uwezo wao kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji na kwamba UNDP itaongeza nguvu kusaidia makundi hayo.
IMG_4033
Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akimwoonyesha eneo maalum lililowekwa uzio kwa ajili ya kulinda mifugo na wanyama wa kali Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez aliyefika wilani hapo kukagua miradi hiyo.
Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha ambaye pia ni mtafiti mkuu wa wanyama katika taasisi ya utafiti wa wanyamapori TAWIRI amesema mradi huo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuanza kupunguza uhasama kati ya wafugaji na wanyama pori wanaokula mifugo yao wakiwemo Simba na Fisi.
Kwa upande wao viongozi na wananchi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Longido Bw James Ole Milya wamesema pamoja na changamoto zinazowakabili wanaendelea kutilia mkazo suala la utunzaji wa mazingira na wanyamapori kwani licha ya kuwa ni asili yao ndio msingi wa maisha yao.
IMG_4039
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (kulia) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati alipotembelea wilaya hiyo kukagua maendelo ya miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP. Kushoto ni
IMG_4057
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akisalimiana na na wanawake wa kimasai mara baada ya kuwasili wilayani Longido kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4064
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya kwa pamoja wakizundua uzio wa kuhifadhia mifugo ya jamii ya wafugaji wilayani Longido wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4070
Muonekano wa uzio utakaotumika kuhifadhia wanyama wasidhurike na wanyama wakali mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
IMG_4111
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4075
Baadhi ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_4121 IMG_4077
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
IMG_4088
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisikiliza maelezo ya zawadi za asali za Nyuki wadogo na wakubwa kutoka kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.

No comments:

Post a Comment