Ajali ya hivi karibuni imetokea viungani mwa mji wa Yola,
mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na
uasi wa wanamgambo wa Jihad.
Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram
wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa
Cameroon . Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji
wa Yola wanasema walisikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .
Baada ya kuanguka ikafuatiwa na mfulurizo wa milipuko ,
kwani inaaminiwa kuwa ilikuwa inasafirisha silaha na zana nyingine za kijeshi
kwa wanajeshi wanaopigana Boko Haram. Haijawa wazi ikiwa mtu yeyote aliekuwa
ndani ya ndege hiyo amenusurika na kifo .
Baada ya kusikia kelele , baadhi ya wanafunzi walianza
kukimbia wakihofia kuwa wapiganaji wa jihad walikuwa wakiwashambulia Hii ni
helikopta ya pili ya kijeshi kuanguka katika mji wa Yola wiki hii.
Wakati huo huo katika eneo la kaskazini kuna taarifa kuwa
mji wa Mubi hauko tena mikononi mwa Boko Haram baada ya askari na vikosi vya
usalama vya eneo hilo, wakiwemo wawindaji kuurejesha tena.
Lakini katika sehemu hii ya kaskazini ya jimbo la Adamawa
bado hali ni mbaya na watu wamekuwa wakiukimbia mji huo ambao makundi ya Jihad
yamekuwa yakijaribu kuuteka
No comments:
Post a Comment