Kuna usemi usemao kuwa kama wanaume wangechukua nafasi ya wanawake kuzaa watoto, leo hii kusingekuwa na binadamu. Na sasa uchungu wanaoupata wanawake wakati wa kuzaa unaweza kuonjwa na wanaume nchini China.
Yalaaaaaa
Hospitali moja kwenye mji wa Jinan uliopo kwenye jimbo la Shandong, linawaonjesha wanaume kwenye kifaa maalum ‘childbirth simulator’ ili kujionea wenyewe kile wake zao huwa wanakutana nacho wakati wa kujifungua.
Machozi yakimtoka mwanaume aliyewekewa mashine ya uchungu wa kuzaa
Watu wengi wanaojitolea kuwekewa mashine hiyo ni waume au wachumba wa wanawake wenye ujauzito.
Mwanaume akisikilizia maumivu makali kama wayapatayo wanawake wakati wa kujifungua
Hospitali hiyo imesema inataka kuwaonesha wanaume jinsi wanawake wanavyoteseka wakati wa kuzaa ili wanaume waheshimu kile wanawake wanakipitia.
Wanaume wengi katika zoezi hilo walilia na wengi waliweza kuhimili maumivu hayo kwa dakika chache tu.
No comments:
Post a Comment