Pages

Thursday, November 6, 2014

PICHA ZINAHUZUNISHA; MAMA AMTUPA CHOONI MWANAE, IRINGA


Na Mwandishi Wetu, Iringa.

 Mama mmoja mjini Iringa aamua kumtupa mtoto wake chooni mara baada ya kumzaa nyumbani.

Mtoto huyo wa kiume aliyezaliwa tarehe 4/11/2014 majira ya jioni na mama huyo na kuamua kumdumbukiza chooni ambapo kisa mpaka sasa anamkwepa mumewe aliyepo safarini asijue kuwa amepata mimba na kuzaa.

Hata hivyo chanzo cha habari kinasema kuwa, mama huyo kwa jina la magdalena limano (32) mkazi wa Iringa anatabia ya kumdanganya mumewe na kutoka na mabwana wengine pindi mumewe akiwa safarini kikazi.
 Wasalia wetu wakimtoto shimoni.

 
 Mtoto akiwa ametolewa shimoni.
Wasamalia wema walifika eneo la tukio.

Mtoto huyo aliyetupwa choon majira ya jioni mara baada ya kuzaliwa na kukutwa asubuhi ya tarehe 5/11 asubuhi akiwa analia ndani ya choo na majirani na kutoa taarifa.

Mpaka sasa mtoto ni mzima wa afya na yupo katika uangalizi mzuri wa hospitali huku mama akishikiliwa na jeshi la polisi akisubiri kupandishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment