Afisa mmoja wa polisi wa utawala nchini Kenya ni miongoni
mwa wanaume waliokamatwa kwa kujaribu kumvua nguo mwanamke katika mtaa wa
Komarock viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Polisi walisema watu wanne walimsingira mwanamke huyo
alipokuwa anaenda nyumbani kutoka kanisani akiwa ameandamana na rafiki yake.
Wanaume hao walijaribu kumvua nguo mmoja wa wanawake hao ila
waliokolewa na wananchi waliokuwa wakielekea makwao.
Wanaume wawili waliokuwa wanawaokoa wanawake hao
walijeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Daily Nation, Kioo cha
basi iliyokuwa barabarani pia kilivunjika katika purukushanio hilo.
Polisi waliofika katika eneo la tukio waligundua kuwa mmoja
wa waliowashambulia wanawake hao alikuwa afisa wa polisi.
Tukio hilo limefanyika siku chache tu baada ya mamia ya
wanawake kuandamana mjini Nairobi kulaani kitendo cha kumvua mwanamke mmoja
mavazi yake yakisemekana kutokuwa na heshima.
No comments:
Post a Comment