Katika kile ninachokiona mimi kama ni kuchanganyikiwa ni kitendo cha Rais wa klabu ya Real Madrid Frolentino Perez kutangaza hadharani kuwa watakua tayari kumuachia mshambuliaji ghali zaidi duniani Gareth Bale kujiunga na klabu ya Manchester United endapo tu klabu ya Man Utd itakubaliana na matakwa yao ya kubadilishana na mchezaji Angel Di Maria.
Siku za hivi karibuni mabosi wa klabu ya Manchester United wameshindwa kujizuia na kutangaza hadharani dhamira yao ya kutaka kumsajili mshambuliajai ghali zaidi duniani raia wa Wales Gareth Bale wakidai kuwa tayari hata kuvunja rekodi ya dunia alimradi kuhakikisha wanainasa saini ya mshambuliaji huyo machachari.
Dhamira hayo ya viongozi wa klabu ya Manchester United inachagizwa na matakwa ya meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal kutaka kumjumuisha kikosini winga wa daraja la juu duniani ili kuongeza ubora ndani ya kikosi chake.
Ikumbukwe kuwa klabu ya Real Madrid ilimuachia mshambuliaji huyo raia wa Argentina kwenye dirisha la usajili lililopita na kumfanya mshambuliajaia huyo kutua United kwa ada ya uhamishao iliyovunja rekodi ya paundi milioni 59.
Lakini mara baada ya mauzo hayo kukamilika kuliibuka hali ya kurushiana maneno baina ya Madrid na Di Maria huku klabu hiyo ikimtuhumu mchezaji huyo kuwa uroho wake wa kutaka kulipwa mapesa mengi ndio uliomfanya ajiunge na United.
No comments:
Post a Comment