Pages

Tuesday, November 4, 2014

RUFAA YA PONDA YATUPILIWA MBALI, KESI YAKE YAAHIRISHWA!

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo imetupilia mbali rufaa ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda iliyopelekwa na wakili wake Juma Nassoro ya kupinga hatia ya adhabu aliyohukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. 



Kesi nyingine inayomkabili kiongozi huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo inasikilizwa na Jaji Augustine Shangwa imeahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment