Kushoto
ni Dkt. Frank Forka ambaye ni mkurugenzi PGCEDC Africa Trade Office
akielezea njia za kufuata kwa mwekezaji kutoka Tanzania anapokuja
kutafuta au kufanya mazungumuzo na wawekezaji wa Kimarekani kwa ajili ya
kuingia nao ubia kwa ajili ya kuwekeza Tanzania. Dkt. Frank Furka
alisema jambo la kwanza muhimu ni kujifunza utamaduni wa wafanyabishara
wa Kimarekani hasa inapokuja kwenye swala la muda, Mambo mengine ya
kuzingatia ni ufafanuzi wa kina na uwazi wa fulsa unayoitafutia
mwekezaji na itakapokuja swali uwe na uwezo wa kulijibu kwa ufasaha.
Caroline
Chang kutoka Maryland Center For Foreign Investment akielezea sheria ya
EB-5 Invester's Program inavyoweza kumnufaisha mwekezaji kutoka
Tanzania anayewekeza nchini Marekani.
Jessca
Mushala Mkurugenzi wa SHINA akielezea wawekezaji kutoka Tanzania
wanahitaji mafunzo kwanza jinsi ya kujieleza, kuandika poropozo na
kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa Kimarekani kabla hajakuja
nchini Marekani. Jessca Mushala aliongezea kwamba anampango wa kumtuma
mmoja ya mwakilishi wa SHINA kwenda Tanzania kufanya semina na
wawekezaji wa Tanzania na kuwapa mafunzo ya nini cha kufanya wanapokuja
Marekani kutafuta wawekezaji wanaotaka kuingia nao ubia.
Kutoka
kushoto ni Mzee Zuberi, Stanslaus Munyaraga Malima na Awadhi Zuberi
Athman wa kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Ltd. Awadhi na
Malima wapo nchini Marekani wakijaribu kujinadi kwa wawekezaji wa
Kimarekani watakaoingia nao ubia kwenye fulsa ya uwekezaji ya umeme wa
jua ikiwemo vifaa vya ujenzi.
Kulia
kwa Jessca Mushala ni Mujuni Joseph Kataraia akielezea kampuni ya Urban
and Rural Engineering Services Ltd na aina gani ya mwekezaji
wanaemtafuta kuingia nae ubia wa uwekezaji wa umeme wa jua na vifaa vya
ujenzi.
Dr..Loleta
Robinson anayejihusiha na bishara ya vifaa vya hospitali na maabara
akielezea uzowefu wake na Tanzania na kuchangia utamaduni wa swala la
muda akijitolea mfano yeye mwenyewe alipokua Tanzania iibidi ajifunze
utamaduni wao muda. Tanzania ukitaka kufanikiwa kilichokupeleka
inakubidi uvumilie swala la muda kwani kuchelewa kwenye vikao ni jambo
la kawaida. Dr. Loleta aliongezea alisema baada ya kufahamu hilo
alichokua akifanya ni kuwahi huku akiwa na kitabu chake alichokua
akikisoma huku akiendelea kuwasubili wahusika. Kulia ni Shaban Mseba
aliyekuja kwenye semina hiyo kutoka New York.
wawakilishi kutoka SHINA wakifuatilia semina
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment