Kufuatia kuripotiwa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na mgogoro wa mpaka uliokuwepo kutokana na madai kuwa kisiwa cha Pemba ni sehemu ya Kenya, Serikali ya Tanzania imetoa taarifa rasmi kuhusiana na mgogoro huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe, amewatoa hofu Wananchi kuwa Pemba ni sehemu ya Tanzania na hakuna ukweli wowote kwamba kisiwa hicho ni sehemu ya Kenya.
Akijibu kuhusiana na suala hilo Bungeni Dodoma leo Membe amesema; “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapata taarifa zozote rasmi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kenya kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Serikali hizi mbili… hususan madai ya kisiwa cha Pemba kilicho ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sehemu ya Jamhuri ya Kenya.. Kisiwa cha Pemba ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kitaendelea kubakia hivyo daima…”
“Wizara yangu iliwasiliana na ubalozi wetu Kenya lakini pia tuliwasiliana na Serikali ya Kenya yenyewe.. kucheki kama taarifa hizi zilizoandikwa kwenye magazeti zina mshiko wa Serikali, balozi wetu na serikali yenyewe ya Kenya hawajui suala hili limetokea wapi” –Membe
Kuhusiana na taarifa za kuwepo meli za kutoka Kenya zinazofanya shughuli za uvuvi katika eneo la Tanzania, Membe amesema; “nitawasiliana na wenzangu wanaohusika.. kuanzia wizara inayohusika na JWTZ ambao ndio wana dhamana ya kulinda bahari yetu ya Indian Ocean waone namna ya kudhibiti na namna ya kuwahakikishia wenzetu wa Kenya kwamba hata baharini kuna mipaka yake”-Membe
Jaku Hashim Ayoub, mbunge wa Baraza la wawakilishi Zanzibar akiuliza swali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment