Leo moja kwa moja kutoka bungeni, aliekalia kiti leo ni
mheshimiwa mama Anna Makinda. Swali la kwanza linaulizwa na Freeman Mbowe na
linahusu wizara ya afya.
Swali: Serikali ina mkakati gani kuongeza watumishi (tasnia
ya afya) (Lorensia Jeremia-Bukwimba)
Jibu: Walau jitihada inaonekana kwa allocation iliofanyika
Swali: Serikali ina mkakati gani kuongeza vitetendea kazi na
vifaa tiba
Jibu:Intergreted logic system itasaidia pia itakuja sheria
ya kulazimisha watu kujiunga kwenye mifuko badala ya hiyari na mifuko italeta
uwezo wa kununua vifaa tiba
Swali: Ukosefu wa wahudumu wa afya unapelekea wasio na ujuzi
kuhudumu na wengi wanaondoka kwenda nchi nyingine (Suzan Lymo)
Jibu: Kimepatikana kibali cha kuajiri wahudumu wapya mwaka
huu, mambo yanaenda vizuri japo malengo ya milenia yanaweza yasifikiwe, lakini
serikali haina uwezo wa kuzuia watumishi kuhama nchi
Swali: Hospitali ya mkoa wa Mara inajengwa kwa kasi ndogo
(Vincent Nyerere)
Jibu: 2011/12, 2013/14 serikali imetoa pesa za kujenga
hospitali ya mkoa wa mara, zinaendelea taratibu za kumpata kandarasi wa kujenga
awamu ya pili
Swali: Awamu ya kwanza iligubikwa na rushwa(Hospitali ya
mkoa wa Mara), serikali itaacha lini kunyamazia watu wanaofanya vitendo hivi
Jibu: Mamlaka ya mkoa ilichukua hatua kwa kuwahusisha
TAKUKURU na BRELA
Swali: Fedha za fidia hazifiki kwa wahusika katika ujenzi
hospitali ya mkoa wa Mara
Jibu: Ilikua milioni 35 lakini zimeongezwa mpaka milioni 100
kutokana na revaluation(ilipita miezi sita)
Swali: Lini serikali itasikia kilio cha wanawake kukamilisha
wodi ya kinamama Kilimanjaro(Grace Kiwelu viti maalumu)
Jibu: Martenity ward ni project kubwa, ni kati ya bilioni 9
na 11. Zilitengwa milioni 700 tu kwa ajili ya shughuli hiyo, lazima kuwe na
namna tofauti
Swali: Mitambo ya usalama bungeni inatoa miozi, haihatarishi
afya? (Shekifu)
Jibu: Haitofautiani na inayotumika duniani kote na haina
madhara kwa afya na haiitajiki kutumia aina ya chakula cha ziada kulinda afya
pia hupelekwa tume ya mionzi kila baada ya miezi mitatu mpaka sita kuhakiki
usalama wake.
Swali: Kwanini wafanyakazi wasipewe nguo maalumu kuwazuia wasipate
mionzi (Shekifu-Lushoto)
Jibu:Serikali imechukua ushauri na itaufanyia kazi
Swali: Toka sakata la escrow lianze, usalama wa wabunge
umekuwa mashakani
Jibu(Makinda): Escrow haina mionzi pia inakusudiwa kujenga
kijiji cha wabunge kulinda usalama wao
Swali: Vipenyo vya kuingilia nchini vinahatarisha usalama
(Sanya)
Jibu: Serikali inafanya tathmini wakati wote wa usalama wa
wabunge na wananchi
Swali: Zoezi la kusajili simu bado kuna tatizo, Je! zoezi
hilo limesaidia nini?
Jibu: Sheria inasema ni kosa la jinai kutumia namba ambayo
haijasajiliwa, zoezi limepunguza kwa kiwango kikubwa uhalifu na kuzima namba
ambazo hazijasajiliwa. Ataebainika faini 500,000 na kifungo miezi mitatu na
hairuhusiwi kuuza laini za simu kiholela.
Swali: Kwanini badala ya kumuadhibu mwananchi, zisibaki
kwenye kampuni kama Dubai na China pia India wanavyofanya?, wapi akalalamike
mteja kutokana na makampuni ya simu?
Jibu:Tatizo kubwa sio kusajiliwa kwa simu lakiini ni
kusajiliwa kwa vitambulisho feki, unaazishwa mfumo mpya na simu zitasajiliwa
upya, Ushauri umechukuliwa na kuna mpango wa kuongeza adhabu kwa watu
kujisajili kwa majina ya watu na kufanyia uhalifu wa kuchangia, nikiri polisi
wana uwezo kushughulikia wizi wa mtandao (cyber crimes)Utapeli kwa kutumia
internet umeongezeka sana, serikali italeta sheria kubwa tatu kudhibiti utapeli
kwa njia ya internet, vyombo havina uwezo wa kufatilia vizuri wizi wa mtandao
lakini pia wananchi wawe waangalifu kuambiwa kuchangia kwa kutumia majina ya
watu maarufu
Swali:Kutumia namba isiyosajiliwa ni kosa, Je sio kosa la
jinai kuwauzia watu nyimbo ambao hawajaomba? (Matha Mlacha-Singida)
Jibu: Sheria inakataza kukata fedha kwa huduma ambayo mteja
hajaomba au hajaitumia, Kuna kituo kitakua kinapokea malalamiko ya wateja
yanayohusu makampuni ya simu
Swali: Miongoni mwa vitu vinavyoleta maendeleo ni
mawasiliano, lini vijijini!
Jibu: Mfuko wa mawasiliano kwa wote una lengo la kupeleka
huduma ya wasiliano kwa vijiji visivyovutia mawasiliano kibiashara, inafanyika
kwa hatua kulingana na fedha zinavyopatikana.
Serikali imeingia mkataba maalamu na Vietel kujenga mkonga
maalumu kufikia vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na mawasiliano
Swali: Serikali inajipangaje kutumia teknolojia ya kisasa
ili wananchi wapate taarifa kwa kupitia simu zao
Jibu: Serikali imefanya mpango wa kujenga mkongo wa taifa
kuunganisha wilaya zote nchini, inaendeela kupeleka mkongo kwa mtumiaji wa
mwisho(last user) na kuanzisha vituo vya mawasiliano
Swali: Mkonga wa taifa umefika lakini kuna tatizo la
internet pia bei za internet kwenye mkonga ni kubwa sana wastani wa 120,000
kulinganisha na 30,000 za makampuni za simu (Rage)
Jibu: Tatizo la Tabora ni mahsusi hivyo nitazungumza na
wewe(Rage) na kuona tatizo pia nampongeza Kafulila kwa kuoa na karibu kwenye
chama-Makamba
Swali: Kituo cha wazee Makulandoto
Jibu: Kina jumla ya wakazi 41 kwa sasa, serikali inatambua
na katika kukabiliana inaendelea kutoa huduma na inatenga fedha kuhudumia wazee
wasiojiweza, ilitegwa milioni 38 ili kuendesha kituo. 2014/15 zimetengwa milioni
28 pia wizara ianatoa wito nchini kuhudumia wazee wasiojiweza katika jamii
Swali: Kwa kua kituo cha wazee Kulandoto kimeanzishwa toka
1975 na majengo yana hali mbaya, je lini serikali watajenga majengo mapya
Jibu: Ujenzi wa majengo mapya ni kutokana na bajeti ya
serikali na mwaka huu 1.7 bilioni zimetengwa kwa ustawi wa jamii, fedha
zikitoka itafanyiwa ukaratibati
Kuhamisha ustawi wa jamii kwa waziri mkuu, ilikua huko na
tunaamini ilipo sasa ni mahala sahihi
Swali: 2008 raisi alitoa ahadi ya maji Isaka na Kagongwa leo
ni mwaka wa sita kutoka ahadi ilipotolewa(Ezekiel Maige)
Jibu: Katika kutekeleza ahadi ya Raisi, mshauri kashapatika
na ataanda usanifu na itakamilika baada ya miezi sita.
Isaka na Kagongwa kuna tatizo la maji, pia mikutano
imeshafanyika na naahidi Kagongwa tutaangalia kisima cha zamani na kukirudisha
katika utendaji mapema
Swali:Kwa kua maji ya ziwa Victoria Kahama lakini mtandao wa
maji uko katikati ya mji lakini pembezoni hamna maji
Jibu: Ni mpango wa serikali kutekeleza kama walivyoahidi.
Swali: Kumekua na mfululizo wa maswali kuhusu ahadi za
raisi, serilikani iliji-commit kutoa taarifa kwenye vipindi vya bunge, mbona
haifanyi?(Mnyika)
Jibu: Waziri alisema atatoa ripoti na mimi nilitoa taarifa
na kama kuna haja ya ripoti zaidi, niko tayari kuitoa(Maghembe)
Swali: Programu ya pili ya maji itachukua muda gani?
Jibu: Maji ni uhai, na programu ya awamu ya pili imeshaanza
kutekelezwa na miradi mingi kwake imekwama
Swali: Waziri wa maji alisema pesa itapatika na halmashauri
zitapelekewa pesa, je ni kweli pesa zimeenda kama alivyoahidi?
jibu: Ni kweli na tutaendelea kuwasiliana na mbunge lakini
ni kweli pesa zimeenda.
Swali: Raisi alitoa ahadi nyingi, ni wakati muafaka kuomba
radhi kwa ahadi ambazo hazijatelekelezwa lwa kuwa muda umeisha
Jibu: Ahadi bado zinaendelea kutekelezwa na muda haujaisha
bado.
Swali: Serikali ina mpango gani na kiwanda cha maliasili
(Ngonyani)
Jibu: Serikali iliuza hisa zote na serikali haiusiki na
kiwanda cha maliasili na jukumu la kulipa watumishi ni la mwekezaji lakini
itaendelea kuwapa malighafi
Swali: Wavuvi wengi wanakwama, kwanini serikali haiwasaidii?
Jibu: Kulingana na sheria ya uvuvi kila chombo hukaguliwa na
afisa uvuvi ikiwemo vifaa vya kujiokoa, wizara kupitia vituo vya ukaguzi huwa
inatoa msaada kwa wavuvi wanaokwama baharini
Serikali 2014/15 itaanza kutoa ruzuku na 2.2 Bilioni
imetengwa na pesa ambayo imeshatolewa ni milioni 400 na inalenga kupata zana
bora na vifaa vya kujiokolea.
Swali: Kumeibuka wizi Momba Tunduma, Je! jeshi la polisi
limekabiliana nalo vipi!
Ni kweli na serikali imechukua hatua zifuatazo-kuongeza
askari, kufuatilia taarifa, kukamilisha kituo cha polisi pia kufanya vikao na
wananchi kuhusika katika ulinzi shirikishi. Jeshi limefanikiwa kuvunja mtandao
wa ujambazi na si sahihi jeshi la polisi halichukui hatua
Swali: Wananchi wametaja baadhi ya askari kuhusika (Silinde)
Jibu: Naomba orodha ya askari waliohusika nichukue hatua.
Swali: Umuhimu wa dawati la jinsia katika jeshi la polisi,
(Kikombe-viti maalumu)
Jibu: Serikali inatambua umuhimu dawati la jinsia japo
haijafikia nchi nzimalakini inajitahidi
Wageni
Wageni wanatambuliwa, kuna wageni wa Hussein Mwinyi kutoka
jeshi, wageni wa Kiboma, wageni 25 wa Laurensia Bukwimba, wageni wa Ezekiel
Wenje, wageni 15 wa Amina wakiongozwa na Ibrahim, wageni waliokuja kwa ajili ya
mafunzo, sabini kutoka St. John, wanafunzi kutoka UDOM.
Matangazo ya kazi:
Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, James Lembeli leo tar 24
kutakua na kikao cha kamati jengo la utawala
Komba anawatangazia wanakamati maendeleo ya jamii kutakuwa
na semina baada ya bunge kusitishwa mchana Pius Msekwa
Mbatia: Naomba kuwasilisha hoja, ofisi yako ilipokea ripoti
maalamu kuhusu Escrow na umiliki. Taarifa hii ilikua siri mpaka
itakapowasilishwa bungeni na turiarifiwa taarifa ya PAC haijakamilika na
tumepata taarifa ripoti hio inagawiwa kama njugu na baada ya kutoa taarifa
polisi wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja na inavyoonekana taarifa hio imeibiwa
na ina muhuri wa katibu mkuu na kwa mujibu wa maelezo taarifa hio imeibwa.
Katiba ya jamhuri 1977 linaainisha bunge lina mamlaka ya
kusimamia fedha za umma, kitendo cha kusambazwa mitaani wakati bado haijatolewa
rasmi inadhiirisha kuna watu wamejipanga kushusha heshima ya bunge. Kwa kua
kumekua na jitihada nyingi zinazolenga kuzuia bunge kushindwa kufanya kazi
yake, kwa kutumia kanuni ya 51 naomba kutoa hoja bunge lisitishe shughuli zake
za sasa na kujadili ripoti hio
Makinda: Hamna hoja hapo na kaeni msome kifungu cha 51,
ofisi ya bunge imeshirikiana na polisi ili muhusika asitoke mpaka aeleze mshine
gani zimetumika naikithibitika amefanya atapata kifungo cha miaka mitatu.
Tukipata taarifa ya polisi tutachukua hatua na hamna ubabe hapa ninaoufanya.
Order paper imebadilishwa hivyo litajadiliwa humu ndani,
nchi inaendeshwa kwa taratibu na kazi inaendelea hivyo hatuwezi kujadili kitu
ambacho hakijaishwa.
MIONGOZO MINGI SANA
Mnyaa: Jambo aliloliomba mbatia na mjadala huu ni mpana na
halihusiani tu na kusambazwa nyaraka na wengi wameshachafuliwa ikiwemo na wewe
kuchukua dola 1,000,000/=, kwa heshima tunaomba uruhusu mjadala huu angalau kwa
nusu saa.
Tundu Lissu: Mheshimiwa spika, nashukuru kwa fursa na kwa
kuwa ni suala la kikanuni, ni vizuri turidhike kama huja ya Mbatia ina haja
kujadiliwa ama laa. Kanuni ya 51: Umeridhika na hili suala na ndio maana umempa
nafasi Mbatia, tunajadili yanayotokea na vizuri jambo lizungumzwe ili hii hali
isafishwe.
Makinda: Naheshimu profession yako lakini pia na wewe
uheshimu taratibu, polisi wanaendelea na wakimaliza spika atapanga.
Ole Sendeka: Kamati itawasilisha lakini jambo hili jambo
hili linahitaji kutendewa haki, nna mashaka, bunge litapata muda gani kusoma
ripoti. Ripoti ipatikane kwa wabunge rasmi ili siku ya kuwakilisha tuweze
kujadili
Makinda: Tunafanya utaratibu mpate ripoti mapema
KUPIGA KURA
(AZIMIO LA BUNGE KUZUIA DHIDI YA USALAMA WA MIONDOMBINU
ILIYOJENGWA CHINI YA BAHARI)
Ndiyooo(Azimio limepita)
Miswada ya serikali, muswada ya sheria ya marekebisho
mbalimbali
KUCHANGIA MUSWADA
Mbaruk: Maoni yangu ni vipengele vilivyoondolewa,
mapendekezo ya mabadiliko ya muswada wa mbolea, ni vizuri kumshirikisha
mkulima. Iwapo supplier anatoa mbolea ilio chini ya kiwango atapigwa faini na
wakala lakini katika sheria pia mkulima aweze kudai iwapo mazao yataharibika
kutokana na mbolea isiyokidhi kiwango. Nashukuru
Murtadh Mangungo: Pamoja na maelezo mazuri yaliyotolewa na
mwanasheria mkuu wa serikali, Kifungu cha 36/3 inampa mamlaka waziri kufanya
uteuzi wa waguzi wa mengi, ningependekeza ungezeko wawe wanatangzwa kuondoa
mkanganyiko, Sheria pamoja na uzuri lakiniKiwango cha faini
(100,000,000-500,000,000) hakina mantiki hasa kwa maeneo ya vijijini ambapo
mbolea ambayo wakala anayo inaweza usifikie hata hio milioni 100, sheria iweke
mkazo kwa waagizaji, uwepo ukaguzi wa kutosha na isije kuwaingiza mawakala
katika mtego.
Wanaothibitisha ubora ni TBS, wenzetu wanaodhibiti magonjwa
waangalie vizuri kabla haijamfikia mlengwa. Kutoza faini kwa waagiza mbegu
ambazo hazifai mpaka milioni 8, mara nyingine mbegu kutoota husababishwa na
matumizi hivyo watumiaji pia waangaliwe. Sheria ya bodi ya ugavi, bodi inaweza
kuanzisha kamati zisizozidi tatu lakini hazijawekewa ukomo ni wa muda gani
hivyo ukomo utamkwe na sheria.
Ahadi ya waziri mkuu kuleta sheria itayoweka sawa sheria ya
kazi, sheria imekuja lakini hamjaileta na hatujui mkutano unaofata utakuwa lini
ni linatakiwa kufanyika kabla ya January. Serikali iweke utaratibu mzuri watu
wote wapate mkopo ikiwemo watu wa stashahada, hatuwezi kujenga kada moja tu ya
shahada.
Mnyika: Sehemu ya 33 ya sheria hii ambayo inafanya
marekebisho ya sheria ya maji safi na maji, marekebisho yanafanya sheria hii
itumike jiji la Dar es Salaam. Kuingiza marekebisho hakukidhi kiu kuondoa
mgongano, kero ya maji Dar ni kubwa mno na miradi ilioanzishwa ina migogoro
mikubwa na kuingiza maneno haya pekee hakukidhi kuondoa udhaifu uliopo katika
miradi ya maji.
Ningependa kupata tamko la serikali, ni kwanini serikali
ilikataa hoja binafsi ya maji na kulidanganya bunge kuwa mambo yote katika
utekelezaji wakati kuna mgongano, raisi aliahidi kuitisha kikao kinachowahusu
mamlaka zote zinazohusiana na maji Dar es Salaam, naomba kauli ya waziri mkuu
ni lini ahadi hii itatimilika. Kwa mujibu wa hotuba ya kambi rasmi ya
upinzani(anaeleza), mwanasheria mkuu wa serikali ameondoa sehemu zote za sheria
ambayo aliyaleta kwa manufaa ya kumpa yeye mamlaka ya kuingilia taasisi mbali
mbali lakini hakutoa sababu, katika majumuisho alisema atakuja kusema sababu.
Kitovu cha maombi haya ni kesi mbalimbali hasa zilizoko ndani ya TANESCO na
benki kuu.
Niliweka taarifa kuwa ESCROW ni mali ya umma na kuomba pesa
zisitolewe mpaka mgogoro utapoisha, katika taarifa ya serikali katika kipindi
kifupi zimetumika 60.9 kulipa kampuni ya uwakili ya Mkono na serikali imesema
kuna mianya inayohitaji kuchunguzwa. Wakati yanalipwa ofisi ya mwanansheria
mkuu ama inaridhia au inakaa kimya.
Tunaomba ofisi ya mwanansheria mkuu inaendelea kusema uongo
bungeni. Ni hatua gani serikali imechukua pale ambapo kuna mgongano wa maslahi
na mianya ya rushwa. Kuna taarifa kuwa mtuhumiwa atawahishwa mahakamani ili
yaje kukingwa hapa kwa kusingizia haya mambo yako mahakamani, kiti chako
kitahusishwa na maharamia.
Wanafunzi hawatapata mkopo kwa sheria kutobadilishwa, kwa
sababu watadai bilioni 12. Rudisheni fedha za umma ili wanafunzi wote wapate
mkopo.
Wizara(Elimu): Muswada unaohusu marekebisho ya bodi wa
mikopo umeondolewa, wakati wizara inasoma makadirio katika fungu la HESLB, kazi
kubwa ya HESLB ni kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu 95,000. Baada ya hapo
itakopesha makundi ya walimu wa stashahada ya ualimu wa hisabati na sayansi,
makundi ya sekondari na shule za msingi
SHUGHULI ZA BUNGE ZIMEAHIRISHWA MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI
No comments:
Post a Comment