Mabadiliko hayo yanaanza Jumatatu tarehe 17 hadi tarehe 30 mwezi huu.
Akitangaza mabadiliko hayo jana jijini Dar es Salaam, Afisa uhusiano wa kampuni hiyo,
Bw. Yahya Mkumba alisema mabadiliko hayo yanatokana na matengenezo yatakayokuwa
yanafanyika eneo hilo.
Akielezea zaidi, alisema magari yatakayokuwa yanaelekea Ubungo kutokea Jangwani
yatalazimika kutumia mchepuko uliopo kabla ya kituo cha Magomeni Mapipa kwa kuingia
barabara ya mabasi yaendayo haraka.
Pia magari yatakayokuwa yanatokea Ilala Boma kuelekea Morocco, Ubungo na Jangwani
yatalazimika kutumia barabara moja ya upande wa kushoto.
“Wananchi watuvumilie katika kipindi hiki na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote
utakaotokea,” alisema.
Mradi wa BRT unalenga kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Kilomita 20.9 za mradi huo awamu ya kwanza zipo mbioni kukamilika na kwa mujibu wa ratiba,
zabuni za kupata watoa huduma zinatarajia kutangazwa mapema mwakani.
Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa duniani katika mfumo huo ambao unatarajiwa kuwa
mfano katika eneo hili la Afrika ya Mashariki na kati.
Katika siku za hivi karibuni, viongozi na makundi ya watu mbalimbali yameeleza kuridhishwa
kwao na maendeleo ya mradi huo na kutoa mapendekezo ya kuuboresha zaidi.
No comments:
Post a Comment