Martha Mboma na Saphyna Mlawa
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi, amefunguka kuwa, yupo
tayari kwenda kuitumikia Stand United.
Mshambuliaji huyo amesema yeye hana kikwazo endapo tu timu
hizo mbili zitakubaliana.
Straika huyo kwa sasa hana nafasi katika kikosi cha Yanga
ambayo alijiunga nayo akitokea Mtibwa Sugar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Bahanuzi alisema yupo
tayari kwenda kuitumikia timu hiyo
ingawa na yeye taarifa za kutakwa kwake
amekuwa akizisikia katika vyombo vya habari tu.(P.T)
Straika huyo alisema kuwa si kwa Stand pekee, hata kama kuna
timu nyingine itataka huduma yake isisite kukutana na uongozi wa timu yake ya
sasa.“Nipo tayari kwenda kuitumikia Stand United na timu nyingine yoyote ambayo
itanihitaji lakini kikubwa ni lazima waongee na kukubaliana na uongozi wa Yanga
kwa sababu bado nina mkataba nao.
“Sibagui timu kwa sababu kikubwa ni kupata nafasi ya kucheza
na kuendeleza kipaji changu na soka ndiyo ajira yangu kubwa,” alisema
Bahanuzi.Ikumbukwe straika huyo mwaka 2012 alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
No comments:
Post a Comment