Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha
mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika
mezani, umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuibatiza chumvi
jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko, kiuongo hiki kinaweza kuwa na madhara
pale ambapo inatumika kuliko kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji .
Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako?
Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa kiwango fulani kwani
inasaidia kuongeza madini ambayo mwili wako unayahitaji hatari ni pale
unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji.
Imegundulika kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikizo
la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya
shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo, inashauriwa
utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya.
Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida?
Hupaswi kula zaidi ya gramu tano za chumvi kwa siku, hii ni
sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina ujazo wa miligram 5, inajumuisha
chumvi ambayo unaongeza ukiwa unapika jikoni, chumvi unayoongeza mezani wakati
wa kula na ile chumvi ambayo inapatikana kwenye chakula kiasili hii ni kwa
sababu kuna vyakula ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha ya
chumvi kama vile mikate, Sausage na nyama za kusaga, supu ya kutengenezwa
kiwandani, vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa
(breakfast) na hata baadhi ya biskuti.
Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida?
Waafrika wengi huwa na kasumba ya utumiaji wa chumvi kwa
kiwango kikubwa kuliko kawaida na hii imezoeleka sana kuanzia majumbani mpaka
mahotelini.
Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati
wa milo ya kila siku.
Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu ni chumvi
inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa viwandani ambayo
huwekwa wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko huko viwandani ili
kuvifanya vikae kwa muda mrefu, nusu nyingine ni ile ambayo ambayo huongezwa
jikoni na ile ambayo watu huongeza mezani wakati wa kula ili kukoleza ladha ya
chakula husika.
Nini kinatengeneza chumvi?
Chumvi inatengenezwa na vitu viwili ambavyo ni sodium na
chloride, sodium ni sehemu ya chumvi ambayo ambayo huongeza presha ya damu au
kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza shinikizo au msukumo wa damu hasa pale
unapotumia chumvi nyingi kuliko kiwango cha kawaida, taarifa zinaoandikwa
kwenye vihifadhi vya vyakula hasa vile ambavyo vinatengenezwa viwandani
huonyesha kiwango cha madini ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi, kijiko
kimoja cha chai mara nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium.
Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi
kwenye vyakula ?
Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja
au ghafla , mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya nyingine .
Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina
ladha hata pale ambapo chumvi haijakolea
Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi mezani hatua ya
kwanza ni kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa chakula ,
hii ni kwa sababu unapaswa kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi tangu jikoni
hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani .
Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi unachoongeza wakati
wa mapishi yako, unapaswa kuonja wakati ukiwa unapika ili kuepuka kuongeza
kiwango cha chumvi ambcho kinaweza kuwa
hatari kwa Afya yako, kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake kuna
chumvi ya asili hupaswi kuongeza chumvi nyingine juu yake.
Katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni imefahamika kuwa
kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama chuimvi ambavyo havna madhara
sawa na ya chumvi kwenye mwili wa mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na
ndimu.
Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye
chakula chako ni mdalasini .
salt
Unataka kujua vyakula visivyo na chumvi nyingi?
Vyakula ambavyo havijatengenezwa kiwandani kwa maana ya
vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi nyingi na hii inamaanisha kuwa
unapaswa kuchagua vyakula vya asili kuliko vile ambavyo vimetengenezwa
viwandani.
No comments:
Post a Comment