Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia
mtaroni na kuziba njia.
Basi la abiria lenye
namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga
mapema leo baada ya kutumbukia.
Hali hii imesababisha
foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa
mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata
hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote
wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo.
Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa
balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu
aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment