"Jakaya Kikwete anaingia ameingia katika mwaka wake wa
mwisho wa uongozi wake akiwa na mtihani mkubwa unaohusu ‘legacy’ yake mwenyewe.
Ni Kiongozi pekee wa Tanzania aliyeruhusu taasisi za Uwajibikaji kufanya kazi
zake na hata yeye kujikuta akichukua hatua kulingana na maamuzi ya taasisi
hizo. Kabla yake, hakuna Rais wa Tanzania aliyetoa nafasi kwa Ofisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya kazi zake kwa uwazi na umahiri.
Hatua yake ya kujadili kwa uwazi taarifa ya CAG ya mwaka unaoishia Juni 30,
2006 kwa kuwaita Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya,
kasha Makatibu
Wakuu, Ma RAS na Ma DED ilijenga msingi mkubwa wa taarifa zinazofuata za CAG.
Mwaka 2012 alifukuza kazi mawaziri 6 na manaibu mawaziri 2 kufuatia Taarifa za
Kamati za Bunge za Mahesabu zilizotokana na Taarifa ya CAG.
Haikupata kutokea katika historia ya nchi yetu Rais kufanya
hivyo. Hata hivyo, Rais Kikwete amepata changamoto kubwa inayotokana na
mafanikio yake ya miaka 9 ya uongozi wake. Namna atakavyo shughulikia suala la
akaunti ya Tegeta Escrow, ama itafuta ‘legacy’ yake au itaiimarisha.
Akiimarisha atakuwa ‘redefining leader’ – Kiongozi ambaye anatoa changamoto
kwenye mazoea na kufanya yale ambayo wenzake walishindwa."
Soma RaiaTanzania kesho Jumatatu katika jarida la Elimu.
Hiki ni kitabu changu cha mwisho wa mwaka huu 2014 The Myth of The Strong
Leader by Prof. Archie Brown
No comments:
Post a Comment