Timu ya Barcelona
Shirikisho la soka dunia FIFA limeitupilia mbali rufaa
iliyokatwa na klabu ya Barcelona kuhusu kuizuia kusajili kwa kukiuka kanuni ya
usajili.
Barca walifungiwa kwa miezi 14 kusajili baada ya kufanya
makosa kwa kusajili kinda wa chini ya miaka 18, Ikiwa ni kinyume na kanuni za
usajili za Fifa.
Kwa maamuzi haya timu hii haitakua na uwezo wa kusajili
mchezaji mpya mpaka Januari 2016.Barcelona wantarajia kukata rufaa tena maamuzi
haya ya Fifa kwenye mahakama ya usuhuhishi michezoni(Cas).
Miamba hiyo ya soka ilifanikiwa kuwasajili mshambuliaji Luis
Suarez , mabeki Thomas Vermaelen Jeremy Mathieu golikipa Claudio Bravo na
kiungo Ivan Rakitic mwanzoni mwa msimu baada ya baada ya kupewa ruhusa maalumu
na Fifa.
No comments:
Post a Comment