Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, December 13, 2014

CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YAZOA MAELFU

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo


Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huo
Twanga akionyesha uhodari wa kuchezambele ya mza kuu
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa
 Kada wa CCM Haji Manara  akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo. wa  kufunga kampeni za uchaguzi wa  serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa jimbo la  Ilala ni sehemu salama sana kwa CCM kwa kuwa jimbo hilo lina historia ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa  kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Azani Zungu akilonga jukwaani, ambapo aliwataka watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo kwa kuwa ni eneo la biashara tu, hivyo watendaji hao watengeneze mazingira mazuri badala ya timua timua ya mara kwa mara
Nape akihutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia wananchi kwenye mkutano huo na ifuatayo ni habari kamili ya alichosema

Nape akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika leo  kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Nape akimsikiliza Gungu Mohamed Tambaza akiomba kura
Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape wakati wa mkutano huo
Nape akimpongeza Haji Manara 
Mkotya na Zungu
Mkotya na makada wengine wa CCM wakifuatilia
Shamrashamra uwanjani baada ya mkutano. Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment