Daktari anayetumia pampu ya baiskeli kulifurisha tumbo la
mwanamke anayetaka kukatwa kizazi nchini India.
Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa
kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka
pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa
wanafanyiwa operesheni hizo.
Daktari Chandra Rout, aliyetumia pampu hiyo kwa wanawake 56,
Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo hutumiwa sana katika jimbo hilo
la Orissa.
Maafisa wa serikali walisema gesi ya kaboni, ndio inapaswa
kutumiwa kwa operseheni hizo wala sio pampu za kuweka hewa baiskeli.
Maafisa hao wamesema kuwa watu wanaweza kutumia hewa ya
kaboni lakini utumizi wa pampu hiyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu.
Mwezi Uliopita ,kashfa nyingine ilizuka kuhusu ukataji wa
kizazi baada ya wanawake 15 kufariki walipofanyiwa upasuaji katika jimbo
jengine.
Madawa ya kulevya yalitumika wakati wa upasuaji huo katika
jimbo la Chhattisgarh.
Kambi za ukataji kizazi hufanyika mara kwa mara ili kuwakata
kizazi kwa pamoja wanawake nchini India kama mojawapo ya mipango ya kudhibiti
ongezeko la idadi ya watu nchini humo.
Ripoti kwamba daktari Rout alitumia pampu ya baiskeli ili
kuyafurisha matumbo ya wanawake kwa lengo la kupata nafasi ya vifaa vya
upasuaji kuingia ndani, imezua pingamizi nchini India tangu habari hizo
zitangazwe.
Maafisa wa serikali wamesema kuwa utumizi wa hewa ya kawaida
badala ya ile ya kaboni unaweza kusababisha magonjwa kadhaa.
Mkuu wa afya katika jimbo la Orrisa Arati Ahuja amesema kuwa
ukataji wa kizazi katika jimbo hilo sasa utafanyika katika hospitali zenye
vifaa vyote .
''Madaktari watalazimika kuambatana na maagizo ya kimataifa
ili kukinga maambukizi yoyote '',bi Ahuja alsema.Ukataji wa kizazi hufanyika
kupitia kuzifunga tubu zinazobeba mayai ya mwanamke .
Hii hufanyika kupitia kufunga na kamba na baadaye kukata tubu
hizo,swala linalozuia mayai na mbegu za kiume kukutana ili kutengeza mimba.
Lakini daktari Rout amesema kuwa amekuwa akitumia pampu kwa
zaidi ya mara 100 lakini hakujawahi kutokea tatizo lolote.
Anasema kuwa waliamua kutumia pampu hiyo wakati kifaa kinachojulikana
kama Insafleta kilipokosekana kwa upasuaji.
No comments:
Post a Comment