Wanasayansi wanadai kuwa dawa mpya iliyozinduliwa ya mpango
wa uzazi kwa wanaume imefanikiwa kwa asilimia 99.
Dawa hio imetengezwa kutoka kwa mmea ujulikanao kama
Gendarusa ambao wanaume wa kisiwa cha Papua wamekua wakitumia kujizuia
kuwashikisha wake zao mimba.
Mmea huo unasemekana kuwa na madini ambayo yanatatiza uwezo
wa mbegu za kiume kuzalisha kwa kuzimaliza nguvu na pia kuzifanya kutoweza
kuingia katika mayai ya mwanamke.
Profesa Bambang Prajogo, mtafiti mkuu wa mradi huo anasema
ana furaha sana kuripoti kwamba dawa hio itaanza kuuzwa mwaka 2016 baada ya
miaka mingi ya utafiti na majaribio.
Ingawa dawa hio ya mpango wa uzazi kwa wanaume ina athari
zake, kama vile wanaume kuongeza uzazi wanapoitumia wanasayansi wanaamini kuwa
athari hizo ni ndogo sana ikilinganishwa na dawa zinazotumiwa na wanawake kwani
hauthiri sana homoni zao.
Dawa hio inaweza kumezwa saa moja tu kabla ya tendo la ndoa.
Lakini wazee wa jamii hio huchanganya dawa hio na chai na kuinywa dakika
thelathini kabla ya tendo la ndoa
Hata hivyo wanaume wanaambiwa wasiwe na wasiwasi kwani
wanapata uwezo wa kuzalisha tena siku thelathini baada ya kusitisha utumizi wa
dawa yenyewe.
No comments:
Post a Comment