Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 15, 2014

DIAMOND LAWAMANI MOMBASA, ADAIWA KUWAFUKUZA NYOTA NDOGO NA WASANII WENGINE KWENYE VIP LOUNGE


 Mashabiki wa kike wa Mombasa wakimsonga Diamond kwenye show yake mjini humo weekend iliyopita
Kunyanyashwa kwa wasanii wa Kenya, kumemfanya Diamond na waandaji wa show yake ya Mombasa weekend iliyopita kutupiwa lawama na wapenzi wa muziki nchini humo.
Mtandao wa Standard Media wa Kenya, umeandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.
Mashabiki wa Diamond mjini Mombasa wakifurajia show yake

Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake.
Tukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani 


waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.
“Kama hili likiendelea, wapenzi wa muziki wa Mombasa watagomea show za Diamond mbeleni. Ni fedheha kwa wasanii wetu kutendewa hivyo nyumbani,” alisema Hassan Faisal wa Coastal Films.
Bongo5 haijaweza kuthibitisha mara moja taarifa hiyo kutoka kwa wahusika.

No comments:

Post a Comment