Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama
anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti
hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma
maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au
Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima,
wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao
watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu
chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo
nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya
kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda
pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo
Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18,
mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa
kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa,
bado nahitaji kujitangaza zaidi.”
Zari na Diamondi wakibusiana kimahaba.
MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari ambaye ni mama wa
watoto watatu ana msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’ wengine aliwaowahi
kuanguka nao dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na msichana asiyekuwa na
msisimko wa kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na mwanamke mwenye umbo kama la
mwanaume, utapata msisimko gani hapo? Lakini mcheki mtoto alivyong’aa,
anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa karibu yake tu utagundua kwamba umekaa na
msichana mwenye mvuto ambaye kila wakati atakufanya kuwa bize kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni kwamba mwanadada huyo
yupo vizuri kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu ziweze kupiga hatua
sina budi kukaa karibu na mfanyabiashara mwenzangu (Zari) kwa ajili ya
kushauriana biashara ziende vipi.
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara, kuwa karibu naye
naamini nitajifunza mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa mianya mingi ya kufanya
biashara, lakini je, nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo ningeipata vipi?”
Zari na Diamondi wakiwa kwenye pozi.
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond alidai kwamba
mwanamama huyo ni mzuri kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa, watoto wazuri
wananipenda kwa hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na mwanamke asiyekuwa
mzuri, maneno yangeanza kusikikasikika na isingekuwa poa. Mbali na kuwa
mfanyabiashara, kumtumia kama
msaada wa kunitangaza, lakini Zari ni mzuri
bwana. Ni mwanamke ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza kusema kwamba haujawahi
kukutana na mwanamke mzuri kama yeye.
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni kwamba Zari yupo
vizuri kichwani kwa maana ya kujitambua tofauti na wanawake wote aliowahi
Mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful
Onyinye’.
“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti lakini kwa Zari, ni
mwanamke mwenye hekima na anajitambua sana. Si mzungumzaji kivile na huwa
anapenda kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili yake ameielekezea
kwenye fedha zaidi. Hapendi masihara na fedha, anapenda kujitoa na ni
mchakarikaji sana. Nampenda mwanamke wa hivyo kwa kuamini kwamba atanifanya
nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za warembo wakali Bongo
aliowahi kutoka nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema na mtangazaji
wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, aliwachambua mmoja baada ya mwingine
na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini hawamfikii Zari.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UTAMBULISHO KESHO DAR LIVE
Mbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa huyo alidai
kwamba atamtambulisha rasmi kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa
wa Burudani wa Dar Live, Mbagala jijini Dar atakapokuwa anaangusha burudani ya
kibabe katika Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme mwenzake, Mzee Yusuf na wakali
wengine kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= kwa kawaida na shilingi 20,000/=
kwa V.I.P.
CREDIT: GPL
No comments:
Post a Comment