Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika
Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa
shughuli maalumu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za
Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta
wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo,
huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya
mawaziri na watendaji wa Serikali
waliotajwa katika sakata hilo.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri
wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua
hali ya hewa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu
alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na
kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka
asubuhi kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara
kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu
anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
No comments:
Post a Comment