Pages

Monday, December 1, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMPA MWAKYEMBE MWEZI MMOJA KUTOA MAJIBU KWA NINI MAZAO YA KOROSHO NA UFUTA HAYASAFIRISHWI NJE KUPITIA BANDARI YA MTWARA‏

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  viwanja vya Mashujaa mjini humo akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi wenyewe na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo Katibu mkuu huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Katika kutano huo Kinana amempa wiki mbili Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa mbalimbali hazisafirishwi kwenda nje kupitia bandari ya Mtwara, Lakini pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ni kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao mtwara wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani Mtwara ambako wanafanya shughuli zao, Pia waziri wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja kuhakikisha dampo la taka za sumu zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na viwanda kuacha mara moja kwa sababu zinahatarisha maisha ya wakazi wa Mtwara, Mwisho akaagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa viwanja katika manispaa ya Mtwara kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za kulipa fidia zipo ila kibali kutoka ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MTWARA)
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.


 Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kufurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwahutubia.
 Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji akiwahutubia wapiga kura wake ambao walifurahia sana hotuba yake kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
 Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
 Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape nnauye wakiingia katika uwanja wa mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara leo.

No comments:

Post a Comment