Wakazi
wa Mtwara mjini wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM
ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
ZIARA YA KINANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAINGIZA WANACHAMA ZAIDI YA 40,000 CCM
ZIARA YA KINANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAINGIZA WANACHAMA ZAIDI YA 40,000 CCM
MKUTANO WA HADHARA MTWARA MJINI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia
wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia Serikali kutimiza wajibu
wake kwa wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini na kuwaa
Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu
Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa
vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa
ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini
hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia
katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana kukwamishwa na
viongozi wa juu serikalini.
Wananchi
wakilizunguka gari alilopanda Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye viwanja vya Mashujaa
Mtwara mjini.
MAPOKEZI YA KINANA MTWARA MJINI
Vijana wa Bodaboda wakiongoza
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili
Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na
kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
CCM 2010.
Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya
kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini
ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
MTWARA VIJIJINI
Wananchi wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho
kinachopakana na nchi ya Msumbiji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya kilichopo
mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara
ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kujenga na
kuimarisha chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanguruwe ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria zinazomkandamiza mkulima
inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa mkulima atakuwa
anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima wa korosho.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya
Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara
Vijijini,tarehe 28 Novemba 2014.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa Ahamad Mzee aliyepambana
na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania mwaka 1972 mpakani mwa
Tanzania na Msumbiji.
TANDAHIMBA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia
wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee
ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya
kubangulia Korosho nchini pia aliwataka wazazi wa Tandahimba kusisitiza
elimu kwa watoto wao kwani ndio mkombozi pekee atakayekuja kuwakomboa
kwenye maisha yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia
wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM
na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani
kwa muda mrefu.
Wananchi wa Tandahimba mkoani
Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima
kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya
Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani
Tandahimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba.
NEWALA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF
iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada
ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani
ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa
ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa
Chadema wilaya ya Newala Ndugu Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo
za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape
Nnauye.
Wananchi wakishangilia kurejea
kwa Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu Adam
Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye
viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya
Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima
itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika
nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa
Chadema wilaya ya Newala Ndugu Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa
amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana .
NANYUMBU
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka wilaya ya Nanyumbu
ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na
itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya
vibaya itasemwa.
Wananchi wakimfurahia kumuona mkuu wao mpya wa mkoa.
LULINDI
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe
ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150
kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Wananchi wa
Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati
wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea
nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.
Katibu Mkuu wa
CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya
ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
Kadi
zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari
yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha
Chiungutwa wilayani Masasi.
Wanachama wapya
waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu
wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi
mkoa wa Mtwara.
MASASI MJINI
Wanachama wapya
waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu
wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi
mkoa wa Mtwara.
Wana CCM wakishangilia kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa fisi wilayani Masasi.
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Masasi kwenye uwanja wa
Fisi na kuwataka Watanzania kukiamini chama chao .
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo mjini Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Masasi ambapo aliwaambia
viongozi wajenge utaratibu wa kuwaeleza wananchi maendeleo yao na yapi
yamefanikiwa na wapi hawajafanikiwa, wapi yanakwamishwa.
MKUTANO WA HADHARA LINDI MJINI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia
wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu
waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa
Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda
wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi
Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
RUANGWA
Mapokezi ya Kinana jimbo la Ruangwa
Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
Wananchi wa Ruangwa wakiwa na
mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na
kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza
kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM
kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya
maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu
kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
Mbunge wa Jimbo la Ruangwa
Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea
katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki
shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
LIWALE
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo
aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo
wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.
Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi
ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za
ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya
kazi kwa ufanisi NACHINGWEA
Katibu wa Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia upinzani
umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao kushabikia
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia
kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali inapokosea mambo na kuchelewa
kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso wanapata wananchi, akizungumzia
kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa
maghala na hakuna mtu serikalini amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
MTAMA
Katibu wa NEC Itiakdi na Uenezi
Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chiuta ambapo aliwaambia Chiuta ni
nyumbani na aliwataka watu wachukue tahadhari na vyama visivyo na sera
wala dira
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Chuta ambapo aliwaambia kuwa
maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na kujituma, ambapo aliwaambia kila
nchi itaendelezwa na watu wake.
MCHINGA
Katibu wa Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mchinga mkoani Lindi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Mchinga.
KILWA KUSINI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko
ambapo aliwaambia watendaji wa serikali kutoa elimu ya kuwafahamisha
wavuvi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuchoma vifaa vyao vya kazi,pia
aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kitajirekebisha makosa
yake na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo kwani
jimbo la kusini Kilwa limepotea kutokana na migongano ndani ya CCM,
hivyo basi uchaguzi ujao tujipange vizuri na kurudisha jimbo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko
ambapo aliwaambia kuwa wapinzani hawasemi ukweli unaoendelea kwenye
vyama vyao havisemi kama vimekufa.
Mwananchi akishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
Umati wa wakazi wa kata ya Chumo wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya shule
ya msingi Chumo na kuwaambia kuwa huu si muda tena wa kuwasikiliza
wapinzani kwani upinzani ulishaisha nchini hivyo .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Chumo kwenye viwanja
vya Shule ya Msingi Chumo ikiwa siku ya kwanza ya kuanza ziara yake ya
mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.
No comments:
Post a Comment