Polisi nchini China wanafanya uchunguzi wa kuwasaka mabibi
harusi zaidi ya mia moja wenye asili ya Vietnam ambao walipotea katika kijiji
kimoja masikini kaskazini mwa jimbo la Hebei baada ya kuolewa .
Makuwadi waliowauza mabibi harusi kwa wanaume wameshangazwa
na kitendo cha kupotea kwa mabibi harusi pamoja na pesa walizozipata makuwadi
pia kupotea.
Wanawake hao walikuwadiwa kwa gharama ya dola 16,000 kila mmoja.
Lakini wadadisi wa mambo wanadai kwamba wanaume wa kichina
walioko mijini wanapaswa kuwa na fedha za kutosha ili kuwavutia
wanawake wa Kichina,na hivyo imewalazimu wanaume wa kichina kununua wanawake kutoka nje ya nchi hiyo kama Vietnam,Cambodia na Burma , zoezi linaloonekana kushika kasi kila uchao wakilenga vijiji hohehahe.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment