Mbunge wa chama tawala cha Conservative nchini Uingereza ,
amekiri kucheza mchezo maarufu kwenye tabiti yake wakati wa kikao cha kamati
moja la bunge hilo.
Jarida la The Sun, limechapisha picha za mbunge huyo kwa
jina Nigel Mills akicheza Candy Crush Saga kwenye tabiti yake, wakati wa
mkutano wa kamati hio kuhusu mageuzi ya sera ya serikali kuhusu malipo ya
uzeeni.
Jarida hilo linasema Bwana Nigel alicheza mchezo huo kwa
zaidi ya saa mbili.
Hata hivyo amejitetea akisema alifahamu kilichokuwa
kinaendelea katika kamati hiyo na kwamba lihusika katika kuuliza maswali. Hata
hivyo alikiri kucheza mara mbili na kusema atajaribu kujizuia kucheza mchezo
huo katika siku za usoni akiwa kazini.
No comments:
Post a Comment