Katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara mmoja wa
maeneo ya mazwi kwenye manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, amewatishia
kuwapiga risasi wafanyakazi wa kampuni ya ukandarasi ya Hema Tec, inayotekeleza
mradi wa kuchimba mtaro wa kupitishia mkongo wa taifa wa mawasiliano mjini
humo, kwa kukataa kutii amri yake ya kuwakataza kuchimba kwenye eneo lake, na
wafanyakazi hao kutimua mbio kunusuru maisha yao.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi
wa polisi Lewins Rwegasira, amesema wanamshikilia mtuhumiwa huyo ambaye
amemtaja kuwa Juma Mussa mkazi wa maeneo ya mazwi,
kwa tuhuma za kutishia kuuwa kwa bastola aina ya Browning
yenye namba a 729321, na kuwakimbiza wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Hema Tec
kwa gari lake, ambao waliamua kukimbia baada ya kuona
ameingia ndani na kutoka
na bastola hiyo.
Akiongea na Mwandishi msemaji wa kampuni hiyo ya ukandarasi
ya Hema Tec Bw Abdallah Seleman, amesema mtuhumiwa huyo kwanza aliwakataza
wafanyakazi hao wasichimbe mtaro kwenye eneo hilo, lakini wao wakawaambia
waendelee na kazi kwani wanaitekeleza kwa mujibu wa ramani iliyotolewa na
manispaa ya Sumbawanga, na ndipo alipoamua kuchukua bastola yake baada ya kuona
ameshindwa kupambana na mmojawao aliyemtaja kwa jina la Daud William.
No comments:
Post a Comment