Pages

Monday, December 8, 2014

MSANII DAVIDO WA NIGERIA AONYESHA CHUKI ZA WAZIWAZI KWA WATANZANIA NA TANZANIA KWA UJUMLA MARA BAADA YA MSHIRIKI WA TANZANIA KATIKA BIG BROTHER AFRICA HOTSHOTS 2014 IDRIS SULTANI KUTANGAZWA MSHINDI:

Msanii Davido
Hii ndio tweet ya Davido Muda mfupi tu mara baada ya Idris Kutangazwa Mshindi wa BIG BROTHER AFRICA HOTSHOS 2014.

Na Josephat Lukaza - Wa Lukaza Blog
Mara tu baada ya Idris Sultani Kutangazwa mshindi wa Big Brother Africa hotshots 2014 hatimaye Msanii kutoka nchini Nigeria Davido aonyesha chuki binafsi kwa Watanzania na Tanzania kwa Ujumla mara baada ya kutweet "They Cheat Again lol"  katika ukurasa wake wa tweeter.



Hii inaonyesha wazi kuwa Davido amechukia, na kuumia sana kiasi kwamba akaamua kuonyesha waziwazi chuki zake binafsi kwa kutweet "They Cheat Again lol" Hii inaonyesha wazi kuwa Davido anawachukia sana watanzania na Tanzania kwa ujumla kutokana na Kugalagazwa na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Tanzania Diamond Platnum katika Tuzo za Muziki za Channel O zilizofanyika huko huko Afrika Kusini

Tweet hii imekuja mara tu baada ya Mshiriki Kutoka Nchini Tanzania Idris Sultan kutangazwa Mshindi wa SHindano la Big Brother Africa Hotshots 2014.

Ikumbukwe kuwa Msanii Davido akuweza kuondoka hata na Tuzo moja katika Mashindano hayo ya Channel O yaliyofanyika hivi karibuni Nchini Afrika Kusini 

Tweet hiyo imeonyesha wazi kabisa Davido anachuki binafsi kwa Watanzania na Tanzania mara baada ya kugalagazwa na Staa wa Nyimbo ya nitampata wapi Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment