Wema Sepetu, akiwashukuru mashabiki zake kwa sapoti waliyokuwa wakimpa kwa
kipindi chote cha mwaka mzima 2014, pia alitumia fursa hiyo kumtambulisha
msanii mpya atakae fanya kazi za muziki chini yake.
Msanii wa Bongo Fleva Ally Luna (kushoto),
akiimba wimbo maalum wa kumsifia Wema mara baada ya kutambulishwa kuwa
chini ya Kampuni ya Endless Fame.
Wema Sepetu akitunza Ally Luna.
Wema akiselebuka na meneja wake Martine Kadinda muda mfupi baada ya shoo hiyo kumalizika.
MKURUGENZI
wa Endless Fame Wema Sepetum usiku wa kuamkia leo amemtambulisha msanii
mpya wa Bongo Fleva Ally Luna, kuwa naye atakuwa ni mmoja wa wasanii
wa kampuni hiyo, ambapo atasimamiwa shughuli zote za kimuziki kama ilivyo kwa Mirror.
Tukio la utambulisho wa msanii huyo lilifanyika ndani ya Ukumbi wa Club 71 iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na tukio hilo pia shoo hiyo ilikuwa ni maalumu kwaajiri ya kufunga mwaka kwa kampuni hiyo na kuwashukuru wadau wote waliyokuwa wakiwaunga mkono kwa karibu.
Shoo hiyo ilisindikizwa na wasanii kibao wa Bongo Fleva, akiwemo Bob Junior,Godzilah, Izzo Busnes, Barnaba Boy, Linex na Mirra, ambapo burudani ilikamilika kwa Wema kumtambulisha Ally Luna ma kuwashukuru mashabiki wote waliojitokeza kujumuika pamoja nao usiku huo.
No comments:
Post a Comment