Picha za mtu aliyezikwa ndani ya gari lake la Hummer SUV
jeep nchini Nigeria
Katika siku za hivi karibuni picha za mtu ambaye alizikwa
ndani ya gari aina ya Hummer SUV Jeep nchini Nigeria zimekuwa zikienea katika
mitandao ya kijamii na kuzua mjadala miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo.
Picha hizo zilitoka katika mtandao wa twitter wa msichana
mmoja raia wa Kenya anayetumia jina @Sankorie katika mtandao wake ambaye
alishangazwa na kusema kuwa wanaume wa Nigeria ni matajiri hadi wengine huzikwa
ndani ya magari
yenye thamani ya juu,swala ambalo haliwezi kufanyika nchini
Kenya.
Je, unadhani ni kweli kwamba mtu anaweza kuzikwa ndani ya
gari lake?
No comments:
Post a Comment