Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)MAANDALIZI ya siku ya uhuru
wa Tanganyika (Tanzania Bara) Desemba 9, kutimiza miaka 53, yanaendelea Uwanja
wa Uhuru ambapo kutakuwa na gwaride la kijeshi vikundi vya sanaa, kwaya,
halaiki ya vijana, ‘brass band’ na matarumbeta.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema
milango katika Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambapo
wananchi watakaofika katika hafla hiyo watatumia mlango wa kusini upande wa
Barabara ya Mandela kuingia uwanjani, na waalikwa wenye kadi watatumoa mlango
wa geti namba mbili 2 na viongozi watatumia geti namba tatu 3.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment