Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30
badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo
kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye
utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha
karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwnai long;i yake
iliraruliwa katika mvutano bungeni humo
Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman
Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo
lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo
wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa
bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa
kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya
utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw
augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi
anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria,
mashirika ya
habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au
picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na
wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa
Somalia
Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha
usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya
kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
No comments:
Post a Comment