Ni rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununu
baisekli wengi wakitaka bei nafuu. Nyingi ya baiskeli nchini Uingereza huuzwa
kwa pauni 1,000 shilingi lakini moja na arobaini pesa za Kenya.
Kwa wengi nchini humo hizo ni pesa nyingi sana.
Hata hivyo baikeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu
imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni laki mbili na hamsini au milioni
36,250,000 pesa za kenya. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la
Ferari, kukufahamisha tu.
Gia za baikeli hii zimetengezwa kwa dhahabu
Baiskeli hio ambayo ilitengezwa na kampuni ambayo hutengeza
vitu vya kifahari, Goldgenie imetengezwa kwa dhahabu kutoka kwa mikono na vyuma
vyake vyote. Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24.
Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu
katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli
kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.
Mkurugenzi w akampuni iliyotengeza baiskeli hii anasema
inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo
Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya
kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkrugenzi wa kampuni hio anasema
baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.
"baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni
nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.''
Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,'' aliongeza kusema
mkurugenzi huyo.
Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa,
lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini
itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako
umeiwacha.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment